Kuhusu Taasisi

Taasisi ya Thirdmill ni programu ya cheti iliyoundwa na Thirdmill ili kutoa mafunzo bure, ya seminari, kibiblia na ya kitheolojia kwa yeyote anayependa huduma. Programu hii imeundwa kufanywa katika vikundi vidogovidogo, ambapo ujuzi wa maisha na huduma unasisitizwa kupitia mwongozo wa wakufunzi wa ndani.

Program/ Mpango huu wa Taasisi hutolewa bila malipo na uko wazi kwa kila mtu, bila kujali elimu yake ya awali, na una wepesi wa kutekelezwa kupitia mtandao au nje ya mtandao. Inatumia mtaala wa hali ya juu wa Thirdmill kuwafunza wanafunzi Biblia na theolojia huku pia ikiongeza msisitizo katika matumizi binafsi na huduma. Tunafanya hivi kwa kurahisisha mchakato wa kujifunza na kuongeza hati mahususi zinazokusudiwa kutumika katika mpangilio wa vikundi.

Taasisi ya Thirdmill hufanya kazi na makanisa na viongozi wa Kikristo kuunda jumuiya za mafunzo za ndani zinazojumuisha vikundi vya wanafunzi na mkufunzi wa ndani. Viongozi hawa wa ndani tunawaita Wakufunzi wa Taasisi. Mtaala wetu umeundwa ili kuondoa mzigo wa kuandaa na kufundisha madarasani ili wakufunzi hawa waweze kuzingatia matumizi ya ndani. Kila jumuiya inayojifunza inawajibika kutafuta mkufunzi wake, kwa kawaida huwa ni mtu kutoka kanisa la mtaa, kikundi cha makanisa, au mshirika wa Thirdmill.

Jumuiya zinazojifunza kupitia mbinu ya “mtandaoni” zitaweza kufikia nyenzo za darasani za Taasisi kupitia tovuti ya Taasisi ya Thirdmill. Jumuiya zinazojifunza zinazotumia mbinu ya “nje ya mtandao” zinaweza kuomba kadi ya microSD (kadi ya kumbukumbu) kutoka kwa Taasisi.

Astashahada ya Misingi

Inajumuisha kozi nne za utangulizi kuhusu Biblia na Theolojia

Misingi ya Biblia – pamoja na Beji ya mafunzo kuhusu Uinjilishaji
Ufalme, Maagano & Kanoni ya Agano la Kale, Ufalme & Maagano katika Agano Jipya

Misingi ya Theolojia – na Beji ya mafunzo kuhusu Maombi
Imani ya Mitume, Kujenga/Kuimarisha Theolojia yako

Misingi ya Agano la Kale – na Beji ya mafunzo kuhusu jinsi ya Kufuasa.

Pentatuk (Vitabu Vitano vya Musa)

Misingi ya Agano Jipya – na Beji ya mafunzo ya jinsi ya Kuhubiri/Kufundisha.
Vitabu vya Injili na Kitabu cha Matendo ya Mitume

Astashahada ya Mafunzo ya Biblia

inajumuisha kozi tano za Mafunzo ya Biblia

Vitabu vya Historia katika Agano la Kale – na Beji ya stadi za huduma na maisha.

Kitabu cha Yoshua na Samweli

Manabii wa Agano la Kale – na Beji ya stadi za huduma na maisha.

Kitabu cha Hosea na Somo la ‘Alitupatia Manabii’

Mafundisho ya Paulo – na Beji ya stadi za huduma na maisha
Kiini cha Theolojia ya Paulo na Nyaraka za Paulo akiwa Gerezani

Nyaraka za Agano Jipyana Beji ya stadi za huduma na maisha.

Kitabu cha Waebrania, Waraka wa Yakobo, na Kitabu cha Ufunuo

Ufafanuzi wa Kibiblia – na Beji ya stadi za huduma na maisha

Alitupatia Maandiko: Misingi ya Ufafanuzi wa Maandiko

students learning together

Astashahada ya Mafunzo ya Theolojia

Inajumuisha kozi tano za Theolojia

Mafundisho Kuhusu Mungu – na Beji ya stadi za huduma na maisha.

Kozi ya Tunamwamini Mungu; pamoja na Theolojia ya Kimfumo

Christolojia – na Beji ya stadi za huduma na maisha.
Kozi ya Tunamwamini Yesu: Mafunzo ya Kibiblia kuhusu Utatu wa Mungu

Numatolojia – na Beji ya stadi za huduma na maisha.

Kozi ya Tunamwamni Roho Mtakatifu, na Kujenga Theolojia ya Kibiblia

Anthropolojia & Eskatolojia – na Beji ya stadi za huduma na maisha.

Ufalme wako Uje: Mafundisho kuhusu Siku za Mwisho

Maadili ya Kibiblia – na Beji ya stadi za huduma na maisha.

Kufanya Maamuzi ya Kibiblia

Baada ya kukamilisha Astashada hizi tatu, mwanafunzi atafuzu na kutunukiwa Stashahada ya “Huduma ya Kikristo” (Diploma in Christian Ministry.)

Je, ungependa kuwa Mwanafunzi?

Mahitaji/sifa ya kujiunga: zipo mbili. Moja, Kuwa katika jumuiya inayojifunza. Pili, tunaomba kila mwanafunzi kushirikishwa katika huduma ya kila wiki katika kanisa, shirika au jumuiya ili waweze kuyatumia mambo wanayojifunza katika taasisi/chuo.

Jinsi ya kujiandikisha

Kujiandikisha na Taasisi/chuo bonyeza kitufe KUINGIA DARASANI kilichopo juu ya ukurasa. Kitakupeleka kwenye darasa la mtandaoni la Taasisi, ambapo utaweza kuunda akaunti yako (ya mwanafunzi). ukishakamilisha usajiri, fuata maelekezo ya kujiandikisha katika kila kozi.

Nitapataje mkufunzi?

Njia rahisi za kupata mkufunzi ni kuzungumza na kanisa lako, huduma au jumuiya kuona kama wanaweza kukusaidia kupata mkufunzi. Mara nyingi makanisa yana shauku ya kupata fursa ya kusaidia katika kuwafunza viongozi. Mwanzo mzuri ni kuongea na Wachungaji wa kanisa lako, viongozi au marafiki katika jamii ya kikristo ili kupata wale ambao watapenda/watapendezwa.

Itakuwaje ikiwa sifahamu mtu yeyote kwenye jamii au kanisa anayeweza kujiunga katika hili pamoja nami?

Je unamfahamu mtu yeyote atakayeweza kupenda kuwa mwanafunzi na kujiunga katika kikundi Pamoja nawewe? unaweza kuwa mkufunzi unapopitia madarasa na kupata cheti.

Taasisi imepanga kwa namna ambayo hata kama una uzoefu mdogo sana, bado unaweza kuwa mkufunzi. Tunatoa taarifa zote zinazohitajika ili kuwa mkufunzi, katika ukurasa wetu wa Wakufunzi.

Je! Kama sitapata mtu yeyote wa kuwa naye kwenye hili pamoja na mimi?

Unaweza kuwasiliana nasi na tunaweza kukusaidia kupata mtu katika eneo lako anayeweza kuhudumu kama Mkufunzi au kuwa kwenye kikundi Pamoja nawe. tutumie barua pepe kwa: [email protected]

Kwa taarifa za ziada juu ya jinsi inavyoonekana kuwa mwanafunzi tafadhali tembelea ukurasa wetu wa mwongozo wa wanafunzi.

Unahitaji kuwa Mkufunzi?

Taasisi imepanga kwa namna ambayo mtu yeyote anweza kuwa Mkufunzi.

Kwa vyovyote vile iwe mgeni katika huduma na una uzoefu mdogo au umekuwa katika huduma kwa mda mrefu, unaweza kuwa Mkufunzi. Nyenzo zetu za mafunzo, miongozo ya majadiliano na beji zitakuongoza katika mchakato na mikutano ya kila wiki. Kama una uzoefu wa miaka mingi katika huduma utakuwa na uwanda mkubwa wa kushirikisha uzoefu wako na kama una uzoefu mdogo Nyenzo zetu zitawaongoza katika hatua ambayo wewe na wanafunzi wako mtajifunza na kuzitumia nyenzo hizo.

Kujisajiri kama Mkufunzi fuata hatua zifuatazo, jaza fofu ya usajiri wa Mkufunzi hapo chini.kisha bonyeza kitufe cha “KUINGIA DARASANI” ili kujisajiri katika masomo/darasa la mtandaoni.

Nitakuaje Mkufunzi?

Kuwa mkufunzi ni rahisi. Jiandikishe katika ukurasa huu kwa kutoa taarifa zako hapo chini. Ukishajisajiri kuwa mkufunzi, kuna njia tatu za kupata Nyenzo za mafunzo.

1) Soma muongozo wetu wa Mafunzo, “muongozo wa mkufunzi” na “kanuni za mafunzo ya Taasisi” ambayo unaweza kuichapisha na kuweka kama kumbukumbu au marejeo. Viunganishi vya kupata Hati vipo chini ya ukurasa huu. Bila kujali jinsi unavyopokea mafunzo yetu, miongozo hii miwili daima itatumika kama mwongozo wa kuongoza jumuiya yako katika kujifunza.

2) Tazama video ya mwongozo wa mkufunzi hapo juu, tutaongeza mara kwa mara video zaidi katika siku zijazo.

3) Hudhuria moja ya matukio ya mafunzo binafsi au mtandaoni ya Taasisi ya Thirdmill yanayofanyika mara kwa mara.

Baada ya kufanya moja au haya yote, bonyeza kitufe cha KUINGIA DARASANI kilichopo juu ya ukurasa huu kutengeneza akaunti katika darasa la taasisi na kupata Mtaala.

Fomu ya usajiri kwa mkufunzi

tafadhari weka alama ya nukta mkato kati ya majina.

Orodha ya Fomu

  • Astashahada ya Misingi

  • Astashahada ya Mafunzo ya Biblia

  • Astashahada ya Mafunzo ya Theolojia